Friday, June 14, 2013

branding questions


  1. Brand ni nini?
Ans: Brand ni rasilimali inayotokana na ahadi ambayo inaunganishwa na bidhaa kwa wateja wake.


  1. Kazi za Brand.
Brand  hutambulisha muonekano ,ubora  wa kuaminika kwa watu, huku bidhaa za generic (kawaida)  hazijulikani  na haziaminiki ,hata hivyo brand ni ghali na inahitaji mipango ya muda mrefu

Brand hutofautisha bidhaa na hufanya bidhaa kutambulika mapema

Brand inaruhusu mtumiaji kutengeneza maamuzi na matumizi ya bidhaa

Brand hutengeneza thamani halisi kwenye macho ya washirika wa kibiashara na hupenyeza thamani ndani ya macho ya mtumiaji

Branding hutengeneza trademark ambayo huongeza thamani ya bidhaa.


  1. Kwanini ufanye brand
Unafanya brand kwa sababu unataka kutambulika na kuongeza mauzo

  1. Faida gani unayoipata ukibrand
Brand hukutambulisha,Brand hukutofautisha, brand hutengeneza thamani, Brand hukutengenezea tredemark

  1. Hasara za kutokubrand
Hautajulikana kwenye soko,mauzo yako hayataongezeka,hautapata nafasi kwnye  ushindani

  1. Mifano ya Brand zilizofanikiwa
    1. Steps entertainment (usambazaji muvi)
    1. Msama promotion (matamasha- dini)
    1. Cocacola(Vinywaji)
    1. Kilimanjaro(Maji ya kunywa)
  1. Mifano Brand zilizofeli
    1. General tyre
    1. TOL
    1. Tanganyika peackers
    1. NICO
  1. Brand inasimamiwa na vitu gani?
    1. Nembo
    1. Brand
    1. Utambulisho

  1. Mgawanyiko wa Brand
    1. Brand ya mtu
    1. Brand ya Kampuni/mfumo
    1. Brand ya Bidhaa
    1. Brand ya Alama

  1. Nianze  kufanya nini?
Tengeneza Alama , halafu jibrand uje utengeneze mfumo then bidhaa

  1. Tofauti kati ya kampuni na Brand
Kampuni ni jina la wamiliki wa Brand
Na Brand ni  ahadi unayotaka kuiweka kwa wateja wako, ( ahadi ya mmiliki kwa mteja)
Kutafuta Masoko - ni kujenga brand kwenye akili ya mteja unaemtegemea

  1. Tofauti kati ya elimu ya ujasiriamali na branding
Elimu ya ujasiriamali- ni elimu inayotolewa kwa ajili ya kukutengenezea njia za kujiajiri na kujiongezea mapato.
Elimu ya Branding - Ni elimu ya kujua jinsi ya kuongeza mapato na kujulikana kwenye kipengele chako  cha ushindani

No comments:

Post a Comment