Friday, June 10, 2016

Muonekano wa biashara yako na matokeo yake.

Muonekano wa biashara yako na matokeo yake.

Hali ya mzunguko na mfumo wa biashara imebadilika sana hapa nchini na hii imechangiwa na kuongezeka kwa makampuni ya kigeni ambayo yamekuwa yakiongeza chachu ya kuendelea kufanya zaidi ya pale wazawa wanapofanya, na tofauti kubwa ambayo inafanya kampuni nyingi na biashara nyingi za nje kufanikiwa ni Branding, asilimia kubwa ya hizo kampuni huingia nchini tayari zikiwa zimeshajibrand hivyo inakuwa rahisi kupata nafasi katika soko la ndani.

Kinyume cha hapo asilimia kubwa ya biashara au kampuni zetu wazawa hazijafanya Branding ambayo ndio uti wa mgongo wa biashara, matokeo yake imekuwa hatuwezi kuuza ndani sababu hazina muonekano mzuri na hatuwezi kuuza nje sababu pia hazijafanyiwa branding nzuri.

Baada ya serikali kuiona changamoto hiyo ikaanza kusisitiza wafanyabiashara kufanya branding vizuri( kuboresha  utengenezaji na upakiaji wa bidhaa uwe mzuri na wa kuvutia ili bidhaa zetu zipate nafasi hata katika soko la nje kwa wingi).

Hivyo mabadiliko hayo yameathiri pia na soko la ndani, kwa vile tunaagiza vitu vingi kutoka nje, vile vinavyotengenezwa ndani vikiwa havijabrandiwa vinakosa soko katika eneo lake la ushindani, watu sasa wananunua brand sio bidhaa ukiwaaminisha bidhaa yako ni bora na akaikuta bidhaa yako ni bora basi utakuwa umempata huyo mteja, Je umejibrand vyema kiasi cha kupata nafasi katika eneo lako la ushindani? una nafasi katika soko lako?

Kama bado Karibu Legacy sasa tukubrand kulingana na biashara na eneo lako la ushindani, njoo tukutengenezee stika/lebo kwa ajili ya bidhaa zako ili ujitambulishe vyema,tukutengenezee utambulisho ( nembo) ambayo itakuwalisha kwenye kila bidhaa yako, tukutengenezee vipeperushi muda wa kuandika maelezo marefu ya bidhaa yako umekwisha iweke kwenye dizaini nzuri na watu wataisoma.Karibu sasa ufanye kazi  na watu wanaotambua umuhimu wa biashara yako kwa mteja wako.

Karibu msimu huu wa Ramadhan kuna punguzo kubwa katika bidhaa zetu, maendeleo yako ndio kazi yetu.

Tunahusika na shughuli za Printing, Graphics design, Webtech na Stationeries.Mawasiliano 0713 603699.

Monday, June 6, 2016

Nembo yako inamaanisha nni?

Je wewe ni mfanya biashara au mjasiriamali au mfanyabiashara?umetengenezaje nembo yako? inakidhdi vigezo vya soko lako?

Kwanza Logo ni alama au nembo iliyodizainiwa mahsusi kwa ajili ya biashara yako, inayotumika kukutambulisha nje na ndani ya ofisi. Au Logo ni alama au nembo inayotumika kutambulisha huduma,bidhaa,kampuni au mfumo wowote wa vikundi.

Kwanini biashara yako inahitaji nembo
1.Humpa mteja maana au tafsiri ya biashara yako japo inaweza kuwa sio sawa na ya kwako
2.Huonyesha muonekano unaotakiwa
3.hukuongezea hadhi
4.huonyesha utofauti wako na wengine katika soko
5.Kuwa na muonekano wa kuvutia
6.Hujipanga yenyewe kwa malengo flani ya soko.

Vitu vya kuangalia unapotengeneza logo
1. Iwe ya kipekee
2. Inatakiwa iwasilishe uhalisia wa biashara ,bidhaa au huduma
3. Iwe na uwezo wa kuonekana kwa wateja unaowategemea
4. Iwe na uwezo wa kusimama na kujiimarisha muda hadi muda ( isipitwe na wakati)
5. Iwe na uwezo wa kutumika na kuoneka kwenye kila nyanja yamawasiliano.

Ushindani umeongezeka sana kwa sasa, sokoni bila ya kuwa na bidhaa iliyofanyiwa brand vizuri utalazimishwa kufuata wengine, hivyo hakikisha unafuata mtu au kampuni inayofahamu vizuri branding na( kudizaini ili wakutengenezee nembo itakayokidhi soko na matakwa yake.kwa mawasiliano zaidi 0713 603699 karibu tukutengenezee nembo bora kabisa kwa sasa tuna ofa 3 msimu huu wa Ramadhan.

Tengeneza nembo kwa Tshs.50,000 tu.

Print  business kwa Tshs. 20,000 Kwa piece 100.

Dizaini na kuprint flier/Vipeperushi. =120,000(Fliers 100)

Karibuni.