Je unatambua lebo au stika ya bidhaa yako inahitaji kuwa na vitu gani ili ikupe muonekano sahihi?
Tumepokea wajasiriamali wengi na wafanyabiashara wadogo wengi wakihitaji huduma ya kutengenezewa lebo ama stika kwa ajili ya bidhaa zao, lakini tofauti na ambavyo inatakiwa kuwa asilimia kubwa huja wakiwa na mawazo tofauti kabisa na uhalisia halisi wa stika au lebo inavyotakiwa kuwa.
Lebo yako unayoitengeneza tambua inatakiwa iwe na maelezo ya mmiliki wa bidhaa au brand au brand husika kuwa ndio mmiliki wa brand.mfano wake ni kama ufuatao mmiliki wa soda za Fanta,Sprite na Cocacola ni Cocacola company. Hivyo katika soda za Fanta na Sprite ubavuni zimeandikwa “ a product of Cocacola company” (bidhaa ya kampuni ya cocacola ) lakini katika soda ya cocacola hakuna maandishi hayo ikimaanisha ndio bidhaa mama y azote…Lebo yako inatakiwa iwe na nembo mbili kama mmilika anabidhaa zaidi ya moja au moja kama mmiliki anabidhaa moja tu inayomtambulisha sokoni, hivyo usikimbilie kutengeneza stika ama lebo bila ya kuwa na nembo.
Kitu kingine ni nembo za uhalishaji kama Barcode,TBS na zingine hizi unatakiwa uzipate kutoka sehemu husika ambazo wanatoa ukija kudizaini unakuwa tayari umeshapewa ruhusa ya kuzitumia sio unaemfuata akudizainie ndio akuweke itakuwa kinyume na sheria na mkikamata litakuwa ni kosa la jinai.
Kitu kingine ni kujitahidi kuwa tofauti na wengine brand inatakiwa iwe tofauti hauwezi kupata nafasi katika soko kwa muonekano sawa na wenzako ila kwa kujitofautisha na wenzako, ndio maana makampuni ya simu yote yanatoa huduma zile zile lakini hayafananishi matangazo au ofa .
Karibu Legacy Impresion Company tukudizainie na kukutengenezea muonekano wa tofauti na sahihi katika soko lako la ushindani ili upate nafasi katika macho ya wateja wako…kwa sasa tunaofa nyingi kwa ajili ya msimu wa sabasaba kwa bidhaa zifuatazo Businesscards,Fliers ( Vipeperushi)Stika/Lebo,Nembo,Branding package na vingine vingi wasiliana nasi 0713603699 au info@legacytz.com.
Kuendelea kuona post na kazi zetu like na kushare page hii kwa ofa nyingi zaidi zinazoendelea kila siku www.facebook.com/legacy244